Tenzi Tafsiriwa katika Kiswahili: Ruwaza ya Shujaa Inavyojenga Falsafa katika Utenzi wa Kalevala
No Thumbnail Available
Date
2016
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Nadharia za Tafsiri, Ukalimani na Uundaji wa Istilahi, Daud Publishing Company Ltd
Abstract
Utenzi wa Kalevala ulichapishwa kwa mara ya kwanza kwa Kifini mwaka 1849. Tangu hapo utenzi huo ulitafsiriwa katika lugha zaidi ya arobaini kama vile Kijerumani (1852), Kiingereza (1880), Kirusi (1888), Kihispaniola (1953) na Kiswahili (1992). Hii dhahiri kuwa tafsiri ni moja ya nyenzo muhimu katika maendeleo ya taaluma mbalimbali na mawasiliano ulimwenguni kote. Lengo la makala hii ni kuchunguza namna ruwaza ya shujaa katika utenzi huu, ambao ni kazi muhimu ya tafsiri kwa Kiswahili na katika ushairi wa Kiswahili, inavyojenga na kuibua falsafa katika utenzi huo. Makala hii inatumia nadharia ya ruwaza ya shujaa ya Clyde Kluckhohn (1965) ili kuibua falsafa katika utenzi husika. Data za makala hii zimepatikana baada ya usomaji makini wa utenzi husika pamoja na machapisho mbalimbali yahusikayo. Makala hii imebaini kuwa ruwaza ya shujaa si tu njia ambazo mashujaa katika kazi ya fasihi wanapitia bali pia ni mkabala au nadharia muhimu ya kiuchambuzi wa kazi ya fasihi, hususan utendi.
Description
Keywords
Ruwaza ya Shujaa, Falsafa, Utenzi wa Kalevala