Mwangwi wa Shaaban Robert katika Muziki wa Hip hop na Bongo Fleva nchini Tanzania

No Thumbnail Available
Date
2015
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Mulika, TUKI
Abstract
Shaaban Robert (aliyeishi 1909-1962) ni mmoja wa washairi mahiri wa ushairi wa Kiswahili. Pia, ni mtunzi wa kazi nyingine kama vile insha na riwaya. Umahiri wake unajidhihirisha si tu kwa wingi wa kazi alizotunga, bali pia uteuzi wa fani na maudhui katika kazi hizo. Ingawa alishaiaga dunia muda mrefu uliopita lakini makala haya yanaona kuwa kuna haja ya kuchambua mwangwi wake katika muziki wa Hip hop na Bongo fleva nchini Tanzania. Uandishi wa makala haya umechochewa si tu na umaarufu wa Shaaban Robert, kazi zake na umaarufu wa muziki huu kiasi cha kuwashughulisha watafiti na wanazuoni mbalimbali bali pia kujitokeza kwa vipengele kadhaa vinavyoonekana kushabihiana katika kazi zao za sanaa ingawa wasanii hawa wameishi katika vipindi tofauti. Hivyo basi, madhumuni ya makala haya ni kuchunguza namna wasanii wa muziki wa Hip hop na Bongo fleva wanavyofanana katika baadhi ya vipengele vya tungo zao na Shaaban Robert. Jambo hili limechunguzwa kupitia baadhi ya kazi zao za ushairi na kuchambuliwa kwa kutumia nadharia ya Mwingilianomatini.
Description
Keywords
Mwangwi, Shaaban Robert, Muziki wa Hip hop, Tanzania
Citation