UDSM waja na Suhuhisho la Kielekroniki Kuboresha Usalama wa Barabarani

Abstract
Kwa kuzingatia changamoto zilizooanishwa hapo juu na nyingine, watafiti wa fani ya TEHAMA wa CoICT wakiongozwa na Prof. Nerey Mvungi, Dkt. Honest Kimaro, Prof. Herald Kundaeli, Dkt. Ndyetabura Hamisi na Bw. Mathew Mndeme chini ya ufadhili wa Malamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na usalama barabarani, wanafanya utafiti wa jinsi ya kutumia mifumo ya TEHEMA ili kuchangia katika kutatua matatizo ya utekelezaji wa sheria na kanuni za usalama barabarani. Kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita, CoICT imekutana na wadau mbalimbali kama Wizara ya Mambo ya Ndani na ya Ujenzi na Mawasiliano, Jeshi la Polisi, Sumatra, Tanroad, Costech, TRA, na wengine wengi ili kuelewa mifumo ya taarifa iliyopo na inayotegemewa kutumika. Hali kadhalika, kuona kama kuna uhusiano wa mifumo iliyoko kati ya taasisi moja na zingine, pamoja na changamoto za mifumo hiyo ili kutafuta suluhisho la kitafiti kupitia matumizi ya TEHAMA. Moja ya matokeo ya la utafiti huu ni mfumo wa kielekroniki ujulikanao kama Integrated Road Safety Management System au iROAD kwa kifupi.
Description
Developed inovative system, the Swahili version
Keywords
usalama barabarani, tehama, mifumo ya kielectroniki, usalama ya mali
Citation
Mndeme, et tal, "UDSM waja na Suhuhisho la Kielekroniki Kuboresha Usalama wa Barabarani", Habari Leo, pp 7-8, 29th August 2016