Ujumi wa Mtu Mweusi katika Kazi za Nathari za M.M. Mulokozi

No Thumbnail Available
Date
2018
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Fasihi, Lugha na Utamaduni wa Kiswahili na Kiafrika (Shani Omari na Method Samwel) (wah.), TUKI
Abstract
Mugyabuso Mlinzi Mulokozi ni mwanataaluma mahiri katika fasihi ya Kiswahili na Kiafrika. Ni mtunzi wa kazi mbalimbali kama vile riwaya, tenzi, tamthiliya na mashairi. Hata hivyo, sura hii inaangazia kazi zake za kinathari ambazo hasa zinalenga hadhira ya watoto na vijana. Kazi hizo ni Ngome ya Mianzi (1991), Ngoma ya Mianzi (1991) na Moto wa Mianzi (1996). Vitabu hivi vinahusu mapambano baina ya Wahehe na Wadachi mnamo miaka ya 1891-1898. Tunachunguza namna vipengele vya Ujumi wa Mtu mweusi vinavyojitokeza katika kazi hizo. Baada ya utangulizi huu mfupi, sehemu inayofuata inawasilisha muhtasari wa vitabu teule. Sehemu hii itafuatiwa na fasili ya Ujumi wa Mtu mweusi kisha uchambuzi wa Ujumi wa Mtu mweusi katika kazi teule za Mulokozi. Umuhimu wa Ujumi wa Mtu mweusi kifasihi na kijamii pia unazungumziwa na mwisho kabisa ni hitimisho.
Description
Keywords
Ujumi, Mtu Mweusi, Nathari, Mulokozi
Citation