Athari za Mandhari-lugha kwa Wanaojifunza Kiswahili kama Lugha ya Pili: Mifano kutoka Dar es Salaam, Tanzania

dc.contributor.authorPeterson, Rhoda
dc.date.accessioned2018-11-02T12:08:39Z
dc.date.available2018-11-02T12:08:39Z
dc.date.issued2015
dc.description.abstractWatafiti mbalimbali wamelihusisha eneo la mandhari-lugha na taaluma ya isimu-jamii. Mathalani kutumia eneo hilo kutathmini mwingiliano na mabadiliko ya lugha katika miji mbalimbali ulimwenguni. Pia kuchunguza kiwango cha jamii-lugha ulumbi katika maeneo mbalimbali. Pamoja na hayo, mandhari-lugha inahusiana pia na ujifunzaji wa lugha ya pili. Hii ni kutokana na kuwa eneo hilo linaweza kuwa kielelezo cha kujifunzia lugha kwani linajumuisha vielelezo halisi kama vile picha, maandishi, na wakati mwingine matumizi ya lugha zaidi ya moja. Lengo hasa la makala hii ni kuchunguza athari za mandhari-lugha kwa wanaojifunza lugha ya pili, hususani Kiswahili. Uchunguzi huu unatazamiwa kusaidia kutambua manufaa au madhara yanayoweza kusababishwa na mandhari-lugha katika mchakato wa kujifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Msukumo wa kuandaa makala hii umetokana na kuwa Kiswahili ni lugha inayokua kimatumizi. Lugha hii inatumiwa katika vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni, mikutano ya kimataifa na pia kufundishwa kama somo mojawapo la lugha katika vyuo vikuu mbalimbali ulimwenguni. Hivyo basi, ipo haja ya kufanya tafiti mbalimbali ili kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili.en_US
dc.description.sponsorshipSelfen_US
dc.identifier.isbn9799987531417
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.11810/4956
dc.language.isoswen_US
dc.publisherTUKIen_US
dc.subjectUjifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pilien_US
dc.titleAthari za Mandhari-lugha kwa Wanaojifunza Kiswahili kama Lugha ya Pili: Mifano kutoka Dar es Salaam, Tanzaniaen_US
dc.typeConference Proceedingsen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
CHAKAMA.docx
Size:
347.7 KB
Format:
Microsoft Word XML
Description:
Ripoti ya makala zilizowasilishwa katika kongamano la CHAKAMA
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: