Ukiushi Juu ya Ukiushi- Mchomozo wa Kifonolojia katika Mashairi ya E. Kezilahabi: Mifano kutoka Diwani ya Dhifa

dc.contributor.authorMutembei, Aldin, K.
dc.contributor.authorDzomba, Edwell
dc.date.accessioned2021-05-11T16:23:59Z
dc.date.available2021-05-11T16:23:59Z
dc.date.issued2019-05-15
dc.description.abstractUshairi wa Kiswahili umechunguzwa na wataalamu kadha kwa kutumia mikabala mbalimbali kama vile muundo, lugha, taswira au mkabala wa kiishara, nahata maumbo. Mkabala wa makala hii unaendeleza mjadala kwa kuegemea katika elimu-mitindo. Mkabala wa kielimu-mitindo katika ushairi umewahi kushughulikiwa na wanazuoni mbalimbali waliochunguza mchomozo katika ngazi mbalimbali za kielimu-mitindo kama fonolojia, mofolojia na sintaksia. Dhana ya mchomozo katika tafiti hizi imechunguzwa kwa kuangalia ukiushi wa kaida na marudiorudio ya vipengele fulani katika uwasilishaji wa dhamira mbalimbali katika ushairi. Ushairi wa Kiswahili wa wanausasa umejadiliwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni ushairi unaokiuka kaida zilizozoeleka za utungaji wa mashairi ya Kiswahili. Hata hivyo, kuna mchomozo ambao tafiti zilizotangulia hazikuutilia mkazo katika kuangalia suala la ukiushi. Kwa kutumia Mkabala wa Kielimu-mitindo, makala hii inachambua kimya kama mchomozo wa kifonolojia katika diwani ya Euphrase Kezilahabi, Dhifa (2008). Mashairi haya, kupitia matumizi ya kimya, yanabeba sifa za kipekee ambazo zinatofautiana na sifa za mashairi mengine ya wanausasa. Kwa hiyo, kimya katika mashairi haya kimejadiliwa kama kipengele kinachoonesha ‘ukiushi juu ya ukiushi’ katika ushairi wa Kezilahabi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha vipengele kama ridhimu, onomatopea, takriri, asonansi na konsonansi kama vijenzi vya mchomozo wa kifonolojia.en_US
dc.identifier.citationKiswahili Journalen_US
dc.identifier.issn0023-1886
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.11810/5748
dc.language.isoswen_US
dc.publisherTUKIen_US
dc.relation.ispartofseriesVol. 82;No. 1
dc.subjectMchomozo, Ukiushi, Mashairi ya Kezilahabien_US
dc.titleUkiushi Juu ya Ukiushi- Mchomozo wa Kifonolojia katika Mashairi ya E. Kezilahabi: Mifano kutoka Diwani ya Dhifaen_US
dc.typeJournal Article, Peer Revieweden_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Ukiushi Juu ya Ukiushi.pdf
Size:
81.24 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Main article
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: