Mitindo ya Lugha katika Tovuti za Serikali Nchini Tanzania na Athari zake katika Usambazaji wa Taarifa kwa Umma

dc.contributor.authorKidami, Rhoda P.
dc.date.accessioned2021-04-27T15:40:33Z
dc.date.available2021-04-27T15:40:33Z
dc.date.issued2019
dc.description.abstractTovuti ni miongoni mwa vyanzo vinavyotumiwa na serikali ya Tanzania kusambaza taarifa kwa jamii. Lugha rasmi, yaani Kiswahili na Kiingereza, ndizo zinazotumiwa kwa usambazaji huo. Baadhi ya tovuti zina sehemu ya kuchagua lugha, hivyo, mtumiaji ana uhuru wa kuchagua lugha mojawapo kati ya hizo mbili. Katika makala hii tumechunguza jinsi lugha hizo zinavyotumiwa kwa pamoja kusambaza taarifa kwa umma wa Tanzania na duniani kote kwa ujumla. Kurasa za Kiswahili na za Kiingereza zilizomo ndani ya tovuti moja zimechunguzwa na kubainisha mitindo ya lugha inayotumiwa kisha kutathmini athari za mitindo hiyo katika usambazaji wa taarifa kwa umma. Uchunguzi huo umeongozwa na Mkabala wa Reh (2004) unaohusu aina za maandishi ya kijamiilughaulumbi katika jamii zenye wingilugha. Data zilikusanywa kutoka katika tovuti za wizara za serikali ya Tanzania. Tovuti zilizohusishwa ni zile zenye sehemu ya uchaguzi wa lugha ili kuwezesha ulinganishi wa matumizi ya lugha kati ya kurasa za Kiswahili na zile za Kiingereza. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha matumizi ya lugha mseto kati ya Kiswahili na Kiingereza yaliyopo katika mtindo wa ujalizaji. Mtindo huu ni faafu kwa watumiaji wenye uelewa wa lugha zote mbili ilhali kwa wenye uelewa wa lugha moja, yaani Kiswahili au Kiingereza, watapata baadhi tu ya taarifa.en_US
dc.description.sponsorshipSelfen_US
dc.identifier.issn0856-552X
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/20.500.11810/5685
dc.language.isoswen_US
dc.publisherTUKIen_US
dc.relation.ispartofseriesVol. 17;No. 1
dc.titleMitindo ya Lugha katika Tovuti za Serikali Nchini Tanzania na Athari zake katika Usambazaji wa Taarifa kwa Ummaen_US
dc.typeJournal Article, Peer Revieweden_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Ikisiri.docx
Size:
13.54 KB
Format:
Microsoft Word XML
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: