Browsing by Author "Mutembei, Aldin, K."
Now showing 1 - 3 of 3
Results Per Page
Sort Options
Item Dhana ya Vina na Mizani na Dhima yake katika Ushairi wa Kisasa wa Kiswahili(TUKI, 2020-05-04) Mutembei, Aldin, K.Katika makala hii, tunajadili dhana ya vina na mizani na kuhakiki dhima yake kama inavyojitokeza katika shairi la Kiswahili. Katika kufanya hivi, tumehakiki mitazamo ya pande mbili ambazo mwishoni mwa miaka ya 1960 ziliibua makundi mawili yaliyozusha mjadala mkali kuhusiana na maana ya ushairi wa Kiswahili. Kundi la kwanza linajulikana kama wanamapokeo. Kundi hili lilishikilia kuwa urari wa vina na mizani na kuimbika kwa shairi ni vipengele vya lazima katika kuufanya utungo uwe shairi la Kiswahili; na kundi la pili lilikuwa na mtazamo kuwa vipengele hivyo si vya lazima, na kuwa si lazima ushairi wa Kiswahili uimbike. Kundi hili linajulikana kama wanamabadiliko (au wanausasa). Makala inajadili na kupendekeza mtazamo mwingine wa kuviangalia vina na mizani katika shairi la Kiswahili. Katika makala hii, tumetumia Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji ili kujadili maana aipatayo msomaji wa shairi la Kiswahili kuhusiana na vina na mizani. Makala imejibu maswali mawili: Je, kuna namna moja ya kuangalia maana ya vina na mizani? Je, inawezekana kuwa na vina na mizani katika shairi lisiloimbika? Makala inahitimisha mjadala kwa kudai kuwa ikiwa makundi yote mawili yangeangalia vipengele hivi kiuamilifu, yangefikia uamuzi unaofanana au angalau kukaribiana kuhusiana na nafasi ya vina na mizani katika shairi la Kiswahili. Kwa mantiki hiyo, labda kusingejitokeza mgogoro wa ushairi kama uliotokea.Item The Future of East African Orature in the Digital Age: Kiswahili Narratives in the Social Media(Katedra Języków i Kultur Afryki, Wydział Orientalistyczny, Uniwersytet Warszawski, 2017-09-14) Mutembei, Aldin, K.According to Afroline report (see, http://www.afronline.org/?p=16226), the use of mobile phones in Africa is on the rise. By the end of 2011 there were more than 500 million mobile phone subscribers in Africa. East Africa is one of the leading regions in Africa, not only in mobile phone usage, but also in the way people are interact-ing through various social media. Google, for example, is witnessing growth in the use of internet through cell phones social media connection, where it is reported that four out of every ten Google search requests come from a mobile phone. Through digital devices, users create and share narratives, chats, and send stories and various texts including picto-graphs. Such an increase in the use of digital devices includ-ing TV and mobile phones on the one hand, and the intensifi-cation of interaction through social media on the other have implications on the meaning and structure of narratives, and on Kiswahili orature in general. Given this trend, we can only predict what the future of Kiswahili oral literature could be. Kiswahili, the language that connects East Africans together, has a long tradition of orature. With the advent of digital de-vices, and the unprecedented rate of East African users of such devices, what will the future of Kiswahili orature in East Africa be? Using intertextuality theory, the paper addresses these questions by focusing on Kiswahili oral literature as captured through WhatsApp messenger, an instantaneous messaging application for smartphones.Item Ukiushi Juu ya Ukiushi- Mchomozo wa Kifonolojia katika Mashairi ya E. Kezilahabi: Mifano kutoka Diwani ya Dhifa(TUKI, 2019-05-15) Mutembei, Aldin, K.; Dzomba, EdwellUshairi wa Kiswahili umechunguzwa na wataalamu kadha kwa kutumia mikabala mbalimbali kama vile muundo, lugha, taswira au mkabala wa kiishara, nahata maumbo. Mkabala wa makala hii unaendeleza mjadala kwa kuegemea katika elimu-mitindo. Mkabala wa kielimu-mitindo katika ushairi umewahi kushughulikiwa na wanazuoni mbalimbali waliochunguza mchomozo katika ngazi mbalimbali za kielimu-mitindo kama fonolojia, mofolojia na sintaksia. Dhana ya mchomozo katika tafiti hizi imechunguzwa kwa kuangalia ukiushi wa kaida na marudiorudio ya vipengele fulani katika uwasilishaji wa dhamira mbalimbali katika ushairi. Ushairi wa Kiswahili wa wanausasa umejadiliwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni ushairi unaokiuka kaida zilizozoeleka za utungaji wa mashairi ya Kiswahili. Hata hivyo, kuna mchomozo ambao tafiti zilizotangulia hazikuutilia mkazo katika kuangalia suala la ukiushi. Kwa kutumia Mkabala wa Kielimu-mitindo, makala hii inachambua kimya kama mchomozo wa kifonolojia katika diwani ya Euphrase Kezilahabi, Dhifa (2008). Mashairi haya, kupitia matumizi ya kimya, yanabeba sifa za kipekee ambazo zinatofautiana na sifa za mashairi mengine ya wanausasa. Kwa hiyo, kimya katika mashairi haya kimejadiliwa kama kipengele kinachoonesha ‘ukiushi juu ya ukiushi’ katika ushairi wa Kezilahabi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha vipengele kama ridhimu, onomatopea, takriri, asonansi na konsonansi kama vijenzi vya mchomozo wa kifonolojia.