• Log In
    New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
  • Communities & Collections
  • All of Repository
  • Log In
    New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Mosha, Ernesta S."

Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Uimarishaji wa Ujinsuke katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka katika Hadithi Teule za Kiswahili za Watoto
    (2017) Mosha, Ernesta S.
    Lengo la makala hii ni kuchunguza namna hadithi za watoto za Kiswahili zinavyoweza kutumika kama njia ya kuimarisha ujinsuke1 katika jamii ili kubadili mtazamo hasi kuhusu watoto wa kike na wanawake katika jamii ya Tanzania. Data za mjadala za makala hii zimepatikana kwa kusoma hadithi za watunzi wawili ambao ni Hua (2007) na Mwakoti (2009). Kwa kuongozwa na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji katika uchambuzi wa data za makala hii, inabainika kuwa hadithi zinaweza kutumiwa kuwajengea watoto wa kike mtazamo chanya na uwezo wa kufanya mambo mbalimbali ili kuimarisha usawa katika jamii. Hivyo, hadithi ni njia mbadala ya kuhimiza juhudi na ubunifu kwa watoto wa kike ili kuweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii na kuleta mabadiliko katika mila na desturi zoeleka zinazombagua mtoto wa kike.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Unapoteza wakati wako bure! Hakuna atakayekuamini: Usawiri wa Ubakaji katika Riwaya Teule za Kiswahili
    (2016) Mosha, Ernesta S.
    Makala haya yanajadili tatizo la ubakaji kama lilivyosawiriwa katika riwaya teule za Kiswahili. Kwa kutumia kilongo cha ashiki ya kujamiiana, makala yanaweka wazi mbinu mbalimbali zinazotumiwa na waandishi na kuwafanya wabakaji kuonekana kuwa hawana makosa huku wanawake wanaobakwa wakibebeshwa lawama kutokana na unyanayasaji wanaopata. Mwandishi wa makala anaeleza kuwa usawiri wa aina hii unaendeleza unyanyasaji wa wanawake na unarudisha nyuma juhudi za jamii katika kuleta usawa wa wanawake na wanaume. Athari kubwa inayoweza kutokana na usawiri huu ni kuhalalisha unyanyasaji wa wanawake katika jamii inayolea na kuendeleza vitendo hivi vya kinyanyasaji. Aidha, makala yanabainisha kuwa riwaya zinaweza kutumika katika harakati za kupambana na tatizo hili la ubakaji kwa kusawiri mbinu zitakazowasaidia wanajamii kukomesha ubakaji pamoja na kukosoa vilongo vinavyoendeleza ubakaji kwa kuchomoza na kushadidia vilongo mbadala vinavyowaelimisha wanajamii namna wanavyoweza kuunga mkono harakati za kutokomeza aina hii ya unyanyasaji katika jamii ya Tanzania.

University of Dar es Salaam © 2025

  • RIMS
  • UDSM MAIL
  • ARIS
  • LIBRARY REPOSITORY