Department of Kiswahili Language and Linguistics
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Department of Kiswahili Language and Linguistics by Author "Peterson, Rhoda"
Now showing 1 - 3 of 3
Results Per Page
Sort Options
Item Athari za Mandhari-lugha kwa Wanaojifunza Kiswahili kama Lugha ya Pili: Mifano kutoka Dar es Salaam, Tanzania(TUKI, 2015) Peterson, RhodaWatafiti mbalimbali wamelihusisha eneo la mandhari-lugha na taaluma ya isimu-jamii. Mathalani kutumia eneo hilo kutathmini mwingiliano na mabadiliko ya lugha katika miji mbalimbali ulimwenguni. Pia kuchunguza kiwango cha jamii-lugha ulumbi katika maeneo mbalimbali. Pamoja na hayo, mandhari-lugha inahusiana pia na ujifunzaji wa lugha ya pili. Hii ni kutokana na kuwa eneo hilo linaweza kuwa kielelezo cha kujifunzia lugha kwani linajumuisha vielelezo halisi kama vile picha, maandishi, na wakati mwingine matumizi ya lugha zaidi ya moja. Lengo hasa la makala hii ni kuchunguza athari za mandhari-lugha kwa wanaojifunza lugha ya pili, hususani Kiswahili. Uchunguzi huu unatazamiwa kusaidia kutambua manufaa au madhara yanayoweza kusababishwa na mandhari-lugha katika mchakato wa kujifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Msukumo wa kuandaa makala hii umetokana na kuwa Kiswahili ni lugha inayokua kimatumizi. Lugha hii inatumiwa katika vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni, mikutano ya kimataifa na pia kufundishwa kama somo mojawapo la lugha katika vyuo vikuu mbalimbali ulimwenguni. Hivyo basi, ipo haja ya kufanya tafiti mbalimbali ili kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili.Item Baadhi ya Vipengele vya Uambatizi wa Vitenzi katika Kishambala(TUKI, 2008) Peterson, RhodaUambatizi ni mchakato mmojawapo wa kimofolojia unaohusu uundaji wa maneno. Mchakato huu huhusisha kategoria mbalimbali za maneno, kama vile nomino, vitenzi, vivumishi, vimilikishi, na vioneshi (Kiango, 2000). Vipengele mbalimbali ndani ya kategoria hizo huweza kutofautiana kutoka lugha moja hadi nyingine kutegemeana na sarufi ya lugha husika. Lengo la makala hii ni kuchunguza na kudhihirisha jinsi baadhi ya vipengele vya uambatizi wa vitenzi vinavyojitokeza katika Kishambala. Uchunguzi huu mdogo ni sehemu ya uchunguzi mpana unaolenga kuchambua sarufi ya Kishambala, kazi iliyoanzishwa na wataalamu kadhaa, mmojawapo akiwa marehemu Prof. Besha (1985)Item Mwingiliano wa Lugha ya Mazungumzo na ya Maandishi katika Uandishi wa Kitaaluma wa Insha za Wanafunzi(TUKI, 2012) Peterson, RhodaLugha ya Mazungumzo na ya Maandishi ni njia tofauti za mawasiliano zinazotumiwa na wanadamu. Hata hivyo baadhi ya sifa za lugha ya mazungumzo hujitokeza katika lugha ya maandishi na za lugha ya maandishi hujitokeza katika lugha ya mazungumzo. Mwingiliano huo husababisha uchanganyaji wa miundo ya njia hizi mbili za mawasiliano kwa baadhi ya waandishi. Lengo la makala haya ni: Mosi, kubainisha sifa za lugha ya mazungumzo na ya maandishi hasa katika kipengele cha muundo. Pili, kuonesha mwingiliano wa sifa hizo na sababu zake. Tatu, kutathmini athari za mwingiliano huo katika uandishi wa kitaaluma wa insha za wanafunzi. Inatarajiwa kuwa makala haya yatasaidia kupanua uelewa wa wanafunzi na waandishi kwa jumla kuhusu taratibu za uandishi, hasa wa kitaaluma.