Department of Kiswahili Language and Linguistics
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Department of Kiswahili Language and Linguistics by Author "Kidami, Rhoda P."
Now showing 1 - 4 of 4
Results Per Page
Sort Options
Item Maandishi ya Kijamiilughaulumbi katika Mandharilugha ya Jiji la Dar es Salaam: Aina zake na Mdhihiriko wa Taarifa za Kiisimujamii(TUKI, 2020-07) Kidami, Rhoda P.Matumizi ya wingilugha yanazidi kuongezeka katika mandharilugha ya miji mbalimbali ulimwenguni. Kutokana na ongezeko hilo, ni hali ya kawaida kuona maandishi ya kijamiilughaulumbi katika eneo la mandharilugha. Katika nchi ya Tanzania kwa mfano, tafiti zinadhihirisha kuwapo kwa maandishi ya kijamiilughaulumbi kwenye miji kama vile Dar es Salaam, Arusha, Iringa, Kagera, Manyara na Mbeya. Aidha, maandishi ya kijamiilughaulumbi katika mandharilugha yanaweza kuwa katika aina tofautitofauti kutegemeana na jamiilugha husika. Kwa mujibu wa Reh (2004), maandishi hayo yanaweza kuainishwa katika makundi manne ambayo ni urudufishaji fumbato, urudufishaji usofumbato, urudufishaji achanishi, na ujalizaji. Lengo la makala hii ni kuchunguza aina za maandishi ya kijamiilughaulumbi katika mandharilugha ya jiji la Dar es Salaam kwa kutumia mkabala huo wa Reh (2004). Data zilizotumiwa katika utafiti huu ni maandishi yaliyokusanywa kwa njia ya upigaji picha katika maeneo ya Posta na Kariakoo jijini Dar es Salaam. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwapo kwa aina za ujalizaji pamoja na urudufishaji usofumbato huku aina za urudufishaji fumbato na achanishi zikiwa hazijadhihirika.Item Matumizi ya Lugha katika Mandhari-lugha ya Jiji la Dar es Salaam: Ulinganishi wa Dhima za Kiswahili na Kiingereza(UNAM, 2017) Kidami, Rhoda P.Abstract Numerous studies have been undertaken on the uses of language in the linguistic-landscape of various cities in the world, for instance in Bangkok, Tokyo, Vilnius, Amsterdam, and Gaborone. Those studies revealed that the number of multilingual communities is increasing in the linguistic-landscape, with English use increasing more and more. The question is, what is the language use situation in the linguistic-landscape of Dar es Salaam city? The aim of this paper is to answer that question as well as comparing the functions of Kiswahili and English languages in the linguistic-landscape of Dar es Salaam city. Data were gathered through photographing, interview and observation. The findings of this study revealed the use of seven languages in the area of study. Furthermore, some language functions are similar to both languages (Kiswahili and English) while others are specifically to either Kiswahili or English.Item Mitindo ya Lugha katika Tovuti za Serikali Nchini Tanzania na Athari zake katika Usambazaji wa Taarifa kwa Umma(TUKI, 2019) Kidami, Rhoda P.Tovuti ni miongoni mwa vyanzo vinavyotumiwa na serikali ya Tanzania kusambaza taarifa kwa jamii. Lugha rasmi, yaani Kiswahili na Kiingereza, ndizo zinazotumiwa kwa usambazaji huo. Baadhi ya tovuti zina sehemu ya kuchagua lugha, hivyo, mtumiaji ana uhuru wa kuchagua lugha mojawapo kati ya hizo mbili. Katika makala hii tumechunguza jinsi lugha hizo zinavyotumiwa kwa pamoja kusambaza taarifa kwa umma wa Tanzania na duniani kote kwa ujumla. Kurasa za Kiswahili na za Kiingereza zilizomo ndani ya tovuti moja zimechunguzwa na kubainisha mitindo ya lugha inayotumiwa kisha kutathmini athari za mitindo hiyo katika usambazaji wa taarifa kwa umma. Uchunguzi huo umeongozwa na Mkabala wa Reh (2004) unaohusu aina za maandishi ya kijamiilughaulumbi katika jamii zenye wingilugha. Data zilikusanywa kutoka katika tovuti za wizara za serikali ya Tanzania. Tovuti zilizohusishwa ni zile zenye sehemu ya uchaguzi wa lugha ili kuwezesha ulinganishi wa matumizi ya lugha kati ya kurasa za Kiswahili na zile za Kiingereza. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha matumizi ya lugha mseto kati ya Kiswahili na Kiingereza yaliyopo katika mtindo wa ujalizaji. Mtindo huu ni faafu kwa watumiaji wenye uelewa wa lugha zote mbili ilhali kwa wenye uelewa wa lugha moja, yaani Kiswahili au Kiingereza, watapata baadhi tu ya taarifa.Item Uhusiano wa Kiswahili na Kiingereza katika Muktadha wa Kimandhari-lugha Nchini Tanzania: Uchunguzi Kifani wa Eneo la Mlimani City Jijini Dar es Salaam(UTAFITI, 2018) Kidami, Rhoda P.Various languages are used in Tanzanian linguistic landscape. In addition to others, Kiswahili and English are the main languages that are dominant in terms of usage. Sometimes, these two languages are code-mixed on various linguistic levels, such as on morphemes, words, and sentences. However, language relationship, particularly in the context of written texts, does not end at linguistic levels only. Appearance of writings can also give various relationship information between one language and the other. The main objective of this study was to explore how Kiswahili and English languages relate on the context of linguistic landscape using linguistic features such as morphemes, words, and sentences; and non-linguistic features such as language arrangement within texts, colour usage, and font size. Data which has been used to explore relationship of the two languages were commercial advertisements, which used both Kiswahili and English language around Mlimani City area in Dar es Salaam. Data was analyzed using multimodality approach as proposed by Sebba (2012). Sebba proposes the approach to be used to analyze written texts, particularly those from the multilingual societies. The main argument of the approach is that writings appearance can yield a variety of sociolinguistic information, which cannot be obtained in the spoken texts. Thus, Sebba stresses that analysis of the written texts, particularly those found on language landscapes should include both linguistic features and the appearance of the relevant texts. Results of this study show that Kiswahili and English languages complemented each other content wise on the linguistic landscape within the area of study. Further, other features, such as language arrangement, the use of font size, upper and lower cases, and colour made Kiswahili language more dominant and powerful on the commercial advertisement than English language.