MAHENGE, ELIZABETH GODWIN2018-10-242018-10-2420119789976-9354-1-3http://hdl.handle.net/20.500.11810/4949Kitabu hiki kitatumia nadharia ya lugha kama bidhaa kama inavyotajwa na Bourdieu (1977, 1982, na 1991) kama alivyonukuliwa katika Simmons 2000. Pia tutatumia nadharia ya ‘thamani’ ambayo inaangalia uzuri wa vitu asilia – yaani uzuri wa lugha ya Kiswahili kuwa bidhaa. Katika nadharia hizi, watu wanaelewa thamani ya lugha yao pamoja na lugha nyinginezo ambazo zinatumika katika mazingira yao. Kwa kuzingatia hilo, watu wanafanya uamuzi (uchaguzi) wa kujua lugha gani na kutumia lugha gani katika mazingira husika www.lingref.com/cpp/wss/1/paper1003.pdf. Kwa maneno mengine, nadharia hizi zinaangalia hadhi ya lugha katika maswala ya kiuchumi – je, mtu ajifunze lugha 4 gani na kwa nini. Hapa ndipo suala la uchaguzi au uamuzi wa kujua au kufahamu lugha fulani unapojitokeza. Kitabu hiki itakuwa na sura tatu ambazo ni utangulizi, kiini, na hitimisho. Katika utangulizi tutagusia usuli kuhusu lugha ya Kiswahili ikiwemo nini maana ya ‘uadimu’ wa bidhaa hii ya Kiswahil pamoja na muktadha wa lugha hii katika ulimwengu wa utandawazi. Katika kiini tutazungumzia nadharia za ubidhaishaji na thamani ya Kiswahili pamoja na fursa mbalimbali za kukibidhaisha Kiswahili. Katika sehemu ya hitimisho, tutatoa mapendekezo ya nini kifanyike ili Watanzania waweze kushindana katika dunia hii ya ushindani bila kujitenga au kutengwa.Kitabu hiki kinachambua nafasi ya Kiswahili kama kitega uchumi. Je, bidhaa hii inawezaje kumkomboa na kumtajirisha Mswahili? Jibu la swali hili ni kwamba, kwa kutafsiri kazi mbalimbali zilizoandikwa kwa lugha nyinginezo – kunaweza kumpa soko la ajira mzungumzaji wa Kiswahili. Zipo fursa mbalimbali ambazo zitamwezesha mzungumzaji wa lugha hii kuondokana na umaskini wa kipato. Kitabu hiki kitabainisha kinagaubaga namna ya kutajirika kwa kupitia lugha ya Kiswahili.swKISWAHILI NI AJIRA, KISWAHILI NI BIDHAA, UJASIRIAMALI WA KISWAHILI, KISWAHILI LINGUISTIC MARKETKISWAHILI BIDHAA ADIMU:JIAJIRIBook