Samwel, Method2017-05-252017-05-252013http://hdl.handle.net/20.500.11810/4552Majigambo no moja ya vipangele maarufu katika nyimbo za muziki wa Bongo fleva au muziki wa kizazi kipya. Hata hivyo matumizi ya majigambo katika ushairi wa Bongo fleva yamekuwa yakikemewa na baadhi ya wasanii, wadau na hata hadhira ya ushairi wenyewe. Mmoja wa wasanii waliosimama kidete kupinga majigambo katika ushairi huu ni Selemani Msindi (phk Afande Sele) katika wimbo wake uitwao “Mayowe Part II”. Katika wimbo huo msanii huyo anadai kwamba ushairi wa Bongo Fleva, na muziki wenyewe kwa ujumla, haupaswi kuwa na majigambo bali unaaswa kutoa ujumbe mzito wenye manufaa kwa jamii. Afande Sele anadai kwamba si busara kujigamba juu ya mambo ambayo hujawahi kuyafanya huku kuna matatiizo mengi katika jamii kama vile njaa, UKIMWI, umiskini, uongozi mbaya na kadhhalika ambayo wasanii wangeweza kuyashughulikia katika nyimbo zao. Makala haya yanajaribu kutathmini ikiwa ni kweli majigambo si muhimu katika ushairi wa Bongo fleva. Halikadhalika, yanajadili dhima ya majigambo katika muziki huo.swMuziki, Majigambo, Bongo Fleva, Fasihi ya KiswahiliMuziki si Majigambo, Muziki ni Sanaa si Sawa na Sanaa ya Urembo”: Uhakiki wa Dhima za Majigambo katika FasihiJournal Article, Peer Reviewed