KISWAHILI KWA WAGENI KIONGOZI CHA MWALIMU
No Thumbnail Available
Date
2015
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Eprovin Publisher Company Limited
Abstract
Kiswahili kwa Wageni Kiongozi ch Mwalimu ni kitabu kinachompatia "mwalimu mbinu za ufundishaji lugha ya Kiswahili kwa mgeni. Nneo mgani linamaanisha mtu ambaye si mzawa wa lugha ya Kiswahili, ina maana kuwa, mtu ambaye lugha yake ya kwanza "ya kujifunzia kusoma na kuandika" si Kiswahili. Kitabu hiki ni maalumu kwa Watanzania kwa kuwa asilimia 95% ya watu hawa ni mahiri katika lugha hii yaani waliijua na kuifahamu ugha hii si kwa kujifunza darasani bali ni kwa kutokana na mazingira, muktadha, utamaduni, tajiriba na uzoefu walionao katika jamii. Kwa maneno mengine, "kila" Mtanzania ni "mwalimu" wa Kiswahili kwa mgeni. Kwa hiyo, kitabu hiki kinamfaa mtu yeyote ambaye ni "mmilisi" wa lugha hii na anataka kujikwamua kiuchumi kwa kuwa kitabu hiki kinampatia fursa ya kujiajiri kupitia "bidhaa" hii ya Kiswahili. Kitabu kina mwongozo wa namna ya kumfundisha mwanafunzi anayeanza kujifunza na yule aliyepo katika ngazi ya kati na hata yule wa ngazi ya juu. Pia kitabu hiki kina mfano wa maswali ambayo yanamwongoza mwalimu ili afahamu namna ya kumpima mwanafunzi wa ngazi yoyote. Kitabu kinapatikana kwa shilingi 15,000/= tu. Piga simu 0692825082
Description
Kwa mtu "yeyote" anayetaka kuitumia "fursa" ya kujiajiri kupitia Kiswahili na achangamkie kukisoma kitabu hiki. Ni mtu yeyote kwa maana ya "Msomi" wa kuanzia kidato cha nne na kuendelea akipata mafunzo haya anaweza kumfundisha mwanafunzi wa ngazi ya kwanza ambaye hajui hata namna ya kutamka maneno ya Kiswahili kwa ufasaha. Msomi wa kidato cha sita anaweza kupata mafunzo na kumfundisha mwanafunzi wa ngazi ya kati. Na Msomi wa diploma au shahada anaweza kumfundisha mwanafunzi wa ngazi ya juu anayejifunza Kiswahili. Sharti mojawapo ni kuwa, "yeyote" anayetaka kuwa "mwalimu" wa wageni awe AMESOMA KISWAHILI katika ngazi ya sekondari na AMEFAULU vizuri somo hilo. Karibuni tutengeneze "ajira" na tuwaajiri wengine kupitia "BIDHAA" ya ufundishaji Kiswahili kwa wageni.
Keywords
Kiswahili kwa wageni, jifunze kufundisha Kiswahili ili ujiajiri, Kiswahili ni ajira, Kiswahili ni mgodi wa almasi