Athari za Mandhari-lugha kwa Wanaojifunza Kiswahili kama Lugha ya Pili: Mifano kutoka Dar es Salaam, Tanzania
No Thumbnail Available
Date
2015
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
TUKI
Abstract
Watafiti mbalimbali wamelihusisha eneo la mandhari-lugha na taaluma ya isimu-jamii. Mathalani kutumia eneo hilo kutathmini mwingiliano na mabadiliko ya lugha katika miji mbalimbali ulimwenguni. Pia kuchunguza kiwango cha jamii-lugha ulumbi katika maeneo mbalimbali. Pamoja na hayo, mandhari-lugha inahusiana pia na ujifunzaji wa lugha ya pili. Hii ni kutokana na kuwa eneo hilo linaweza kuwa kielelezo cha kujifunzia lugha kwani linajumuisha vielelezo halisi kama vile picha, maandishi, na wakati mwingine matumizi ya lugha zaidi ya moja. Lengo hasa la makala hii ni kuchunguza athari za mandhari-lugha kwa wanaojifunza lugha ya pili, hususani Kiswahili. Uchunguzi huu unatazamiwa kusaidia kutambua manufaa au madhara yanayoweza kusababishwa na mandhari-lugha katika mchakato wa kujifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Msukumo wa kuandaa makala hii umetokana na kuwa Kiswahili ni lugha inayokua kimatumizi. Lugha hii inatumiwa katika vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni, mikutano ya kimataifa na pia kufundishwa kama somo mojawapo la lugha katika vyuo vikuu mbalimbali ulimwenguni. Hivyo basi, ipo haja ya kufanya tafiti mbalimbali ili kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya pili.
Description
Keywords
Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili