Dhana ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar: Uchambuzi kupitia Lugha ya Kiswahili

No Thumbnail Available
Date
2016-02-15
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Muungano kati ya watu wa Tanganyika na Zanzibar unachunguzwa kihistoria ambapo hoja za kijamii, kisiasa na kiuchumi hutolewa katika kuhalalisha uhistoria wa muungano huo wa kipekee. Ingawa kuna baadhi ya mijadala ya kikatiba kuhusu nguvu za kisheria za muungano, hoja za kiisimu ni mara chache hutolewa ili kuongezea uhalali wa muungano huo unaobishaniwa. Makala hii inatoa mkabala wa kiisimu kuhusu muungano. Kwa kutumia nadharia ya usafiri kama ilivyoelezwa na Edward said (1983), makala inajadili kuenea kwa Kiswahili Sanifu katika Tanzania ambapo kuna lugha zaidi ya 123 huku nyingine zikiwa na sarufi na kamusi zilizoandikwa. Hoja ya Kiswahili sanifu inafafanuliwa zaidi kwa kugawanywa katika vipengele kadha kwa mujibu wa nadharia ya usafiri. Mwishowe makala inaonesha kuwa lugha na fasihi ya Kiswahili huku vikiongozwa na Kiswahili sanifu vinajenga hoja ya nguvu kuhusu muumano na uhalali wa muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.
Description
Keywords
Lugha ya Kiswahili, Fasihi ya Kiswahili, Muungano, Kamati ya Lugha Afrika Mashariki, Nadharia ya Usafiri
Citation
Mutembei, A.K, 2016