Kukitandawazisha Kiswahili kupitia Simu za Kiganjani: Tafakari kuhusu Isimujamii

Abstract
Mojawapo ya matokeo ya utandawazi ni kuwapo kwa simu za kiganjani1 na matumizi yake. Siku hizi nchini Tanzania mawasiliano ya simu yamekuwako kwa wingi kuliko ilivyokuwa tangu wakati wa uhuru hadi katikati ya miaka ya tisini. Mahali ambapo hakukuwa na mawasiliano kabisa, kama sehemu nyingi za vijiji vya Tanzania, siku hizi kuna mawasiliano kwa njia ya simu hizi za kiganjani na lugha inayotumika katika mawasiliano haya ni Kiswahili. Lugha ya Kiswahili inayotumika katika simu hizi ni ya kiutandawazi na pengine si rahisi kuiona nje ya wigo huu wa kiutandawazi ambao pia unajumuisha mawasiliano kwa barua pepe, na maongezi katika tovuti. Katika lugha hii ya kiutandawazi, watu huwasiliana kwa kutumiana matini fupi fupi zenye mchanganyiko wa maneno na namba, na hivyo kuunda lugha tofauti na iliyozoeleka katika jamii nyingine.
Description
Keywords
Citation
Mutembei, A., 2011. Kukitandawazisha Kiswahili kupitia simu za kiganjani: tafakari kuhusu isimujamii.